Wakati mabingwa wa kihistoria Yanga wakisubiri kushuka dimbani kesho Jumapili kuikabili Mbeya City katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom, mechi tatu zinatarajiwa kupigwa katika viwanja mbalimbali
Mtibwa Sugar watakuwa nyumbani mkoani Morogoro kuikabili Simba wakati JKT Tanzania wataumana na Dodoma Jiji katika mchezo wa dabi ambao utapigwa uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma
Mchezo mwingine ni kati ya KMC dhidi ya Tanzania Prisons. Azam Tv wataonyesha mecho zote mbashara

Jana Azam Fc ilifanikiwa kupanda kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kuichapa Coastal Union mabao 2-0 na kufikisha alama sita wakati Gwambina Fc ilitoka suluhu ya bila kufungana dhidi ya Kagera Sugar
Aidha TFF imetangaza kuufungia uwanja wa Gwambina ikiwaagiza wamiliki wa uwanja huo kufanyia marekebisho eneo la kuchezea 'pitch'