Yanga imeweka hadharani viingilio vya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City ambao utapigwa keshokutwa Jumapili kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa
Kiingilio cha chini kabisa Mzunguuko ni Tsh 5,000/- wakati VIP A ni Tsh 15,000/-, VIP B na C ni Tsh 10,000/-
Wananchi wenyewe wanasema huu ndio mchezo wao wa kwanza msimu huu, kwani ndio mchezo wa kwanza watavaa jezi zao mpya
Mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons walitumia jezi za msimu uliopita na ndio maana hata matokeo yalikuwa ya ki-msimu uliopita
Shughuli inaaza dimba la Mkapa Jumapili
ADVERTISE HERE