Straika kutoka Guinea kujaribiwa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Nov 2017
Straika kutoka Guinea kujaribiwa Yanga
Yanga ilikuwa imempa Ngoma mpaka jana Ijumaa usiku awe amerudi kazini akitokea kwao Zimbabwe alikosema anaenda kutibiwa ingawa hawana uhakika kwani aligoma kuwapa vithibitisho.

Lakini habari mpya kutoka ndani ya Kamati ya Usajili kwamba imenasa vifaa vipya viwili na kimoja kitachukua nafasi ya Ngoma ambaye kwa hali ilivyo uwezekano wa kupigwa chini ni mkubwa.

Mabosi wa Yanga wamepewa majina mawili ya mastraika wanaotakiwa kuja kufanyiwa mchujo wa mwisho akiwemo Mguinea, Bensua Da Silva ambaye ana nafasi kubwa ya kusajiliwa kwani wakala wake anasifika kwa kumiliki wachezaji wa maana.

Ingawa uongozi wa Yanga haujaweka wazi, lakini Da Silva kuna uwezekano akasaini, pia kuna Mnigeria atakayekuja wiki ijayo kwa majaribio.

Da Silva ambaye ni mshambuliaji namba moja, inaelezwa kwamba ni mjuzi wa kufunga kwa miguu yote na hata vichwa na anatokea klabu moja ya Togo, lakini vilevile ameitolea nje African Sport ya Ivory Coast.

Katika ripoti yake ya usajili, kocha George Lwandamina, amewataka mabosi wa timu hiyo kuhakikisha anatafutwa mshambuliaji kiongozi kutokana na kikosi chake kujaa viungo washambuliaji (namba 10) akiwa na Ibrahim Ajibu, Obrey Chirwa na Ngoma huku Amissi Tambwe pekee akibaki kuwa mshambuliaji namba moja.

Kwa hisani ya Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’