Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kuwa hafla ya uzinduzi wa jezi kwa ajili ya msimu wa 2020/21, itafanyika kesho Ijumaa, Septemba 11 Makao Makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Twiga na Jangwani
Baada ya uzinduzi, jezi zitaanza kupatikana kwenye maduka yote ya GSM pamoja na duka rasmi la klabu ya Yanga pale Makao Makuu
Jezi zitakazoanza kuuzwa ni Grade A kwa bei ya Tsh 35,000/-
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Simon Patrick amewaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo baada ya jezi kuchelewa kutokana na changamoto ya ugonjwa wa corona
ADVERTISE HERE