Kocha Mkuu wa Yanga Zlatko Krmpotic amedokeza kuwa mchezo ujao wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City, anatarajiwa kuwapa nafasi nyota wa kigeni ambao hawakuanza mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons
Wacongomani Tuisila Kisinda, Mukoko Tonombe, Mnyarwanda Haruna Niyonzima, Mburkinabe Yacouba Soghne na Muangola Carlinhos ni miongoni mwa wachezaji ambao hawakujumuishwa kwenye kikosi cha kwanza cha mchezo uliopita
Sababu kubwa baadhi ya wachezaji kuanzia benchi ni kuchelewa kwa ITC zao, mfano Kisinda na Mukoko ITC zao ziliwasili saa chache kabla ya mchezo huo
Krmpotic amesema Wanayanga watarajie mabadiliko makubwa ya kikosi chake kwenye mchezo wa Jumapili, nyota wa kigeni watajumuishwa
"Mchezo unaokuja utakuwa na mabadiliko ya wachezaji kwenye kikosi cha kwanza, kutakuwa na baadhi ya wachezaji ambao sikuwaanzisha kwenye mechi iliyopita. Nafanya hivyo kutafuta ushindi wa kwanza," alisema Krmpotic.
"Unajua kwenye mchezo uliopita sikuwa na mpango wa kuwatumia wachezaji wa kigeni baada ya kukosekana vibali vyao vya kazi ambavyo vilipatikana mchana ndiyo maana asilimia kubwa niliwaanzisha wazawa lakini mchezo ujao tutawapa nafasi baadhi ya wachezaji ili pia tukate kiu ya mashabiki wetu"
Miongoni mwa wachezaji ambao Wanayanga wanasubiri kwa hamu kuwashuhudia uwanjani ni kiungo Carlinhos ambaye hakupata nafasi kwenye mchezo uliopita