Mshauri (Consultant) wa masuala mbalimbali ndani ya uongozi wa Yanga, Senzo Mazingiza amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuunga mkono jitihada zinazofanywa katika kuisuka upya Taasisi ya Yanga
Senzo aliyejiunga na Yanga akitokea klabu ya Simba ambako alikuwa Mtendaji Mkuu, amesema wakati huu ni muhimu kwa Wanayanga kuwa pamoja kuhakikisha wanajenga Taasisi imara
"Kwa pamoja tuijenge timu yetu, tusimamie misingi yetu na wala tusikubali kuyumbishwa na mtu yoyote. Muhimu pia tuwaunge mkono wachezaji na benchi la ufundi kwani tukiwa wamoja tutafanikiwa," aliandika Senzo kwenye ukurasa wa mtandao wake wa kijamii
Tangu Senzo aanze majukumu yake ndani ya klabu ya Yanga mapema mwezi huu, tayari kuna mambo makubwa yamefanyika
Kwanza tumeshuhudia tukio la kihistoria la kilele cha wiki ya Mwananchi. Mpangilio wa matukio siku ile ulifanya Tamasha zima kuwa la kipekee
Si ajabu kuona klabu ya Aigle Noir ambao walialikwa, walilibeba Tamasha lile kama lilivyo na kwenda kulifanya kwao
LakiniΒ pia hivi karibuni Yanga imehamishia kambi yake kule Kigamboni ambapo sasa timu inaishi mahali pamoja. Yale masuala ya wachezaji kutokea majumbani kwao hayapo tena
Timu inaishi eneo ambalo inapata mahitaji yake yote ikiwemo kiwanja kizuri cha kufanya mazoezi