Kocha Mkuu wa Yanga Zlatko Krmpotic hakumtumia kiungo Carlinhos kwenye mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons, akitaja sababu kuwa nyota huyo aliyetua kutoka Angola, bado hayuko fit
Hata hivyo Krmpotic amewahakikishia Wanayanga kuwa wakati wake utafika, nafasi ya kucheza atapata
Aidha Mserbia huyo ameelezwa kuridhishwa na uwezo wa nyota huyo, lakini muhimu anahitaji afikie 'fitness' inayotakikana
"Sina shaka na uwezo wake, ni mchezaji mzuri, ana kipaji cha hali ya juu, lakini nadhani anahitaji kuimarika zaidi, hayuko tayari kucheza dakika 90. Sio yeye tu, wako wengine pia tunawaangalia, baada ya muda nafikiri tutakuwa na timu imara," alisema
Carlinhos alicheza takribani dakika 10 siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi dhidi ya Aigle Noir
Wanayanga wanaweza kwenye mchezo ujao dhidi ya Mbeya City ambao utapigwa siku ya Jumapili, Septemba 13 katika uwanja wa Mkapa
Kiungo huyo fundi alipata mapokezi ya aina yake wakati akitua Yanga akitokea Interclube ya Angola
Wengi wanashauku ya kumuona akicheza hasa kutokana na sifa zilizotajwa kuwa nazo