Krmpotic aongeza dozi ya mazoezi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Sep 2020
Krmpotic aongeza dozi ya mazoezi

Baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa ufunguzi ligi kuu ya Vodacom juzi, kocha mkuu wa Yanga Zlatko Krmpotic ameendelea kukiandaa kikosi chake kuelekea mchezo wa pili dhidi ya Mbeya City ambao utapigwa Jumapili ijayo

Yanga inajifua huko Kigamboni ilikoweka makazi yake, vijana wakifanya mazoezi mara mbili kwa siku

Katika moja ya changamoto ambazo Krmpotic alibainisha juzi baada ya mchezo, ni kikosi chake kutokuwa na utimamu wa kucheza kwa dakika 90

Krmpotic amewaongezea 'dozi' ya mazoezi wachezaji wake ili kuhakikisha anamaliza changamoto hiyo

Krmpotic anafahamu ashabiki hawatakuwa tayari kupokea matokeo tofauti na ushindi mchezo wa Jumapili

Mserbia huyo anahitaji kuchanga karata zake vizuri ili ahakikishe timu inapata matokeo na wakati huohuo akiendelea kukiimarisha kikosi chake

Kipaumbele cha Yanga msimu huu ni kutwaa ubingwa, kuendelea kuangusha alama mapema kunaweza kuvuruga mipango hiyo

Hili ni jambo ambalo Wanayanga hawatapenda kuliona msimu huu baada ya kuvumilia misimu mitatu bila kutwaa taji lolote

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’