Nahodha wa Yanga Deus Kaseke amesema wachezaji wote wamepania kushinda mchezo unaofuata dhidi ya Mbeya City baada ya hapo jana kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Tanzania Prisons
Kaseke amesema hayakuwa malengo yao kupata matokeo ya sare lakini hawapaswi kukata tamaa
"Sio malengo yetu kwa matokeo jana naamini hatutainamisha vichwa chini tutarudi tukiwa na nguvu hali na morali yakushinda mechi ijayo," aliandika Kaseke kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Kaseke alikuwa mmoja wa nyota 11 walioanza kwenye kikosi dhidi ya Tanzania Prisons
Alitoka wakati wa mapumziko na nafasi yake kuchukuliwa na Yacouba Songne
ADVERTISE HERE