Mbeya City imeanza msimu vibaya kwa kubugizwa mabao 4-0 na KMC katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa mapema leo
Jumapili ijayo Mbeya City watachuana na Yanga katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa Mkapa, saa moja jioni
Kwa Yanga huo ni mchezo ambao wanapaswa kushinda hasa baada ya kulazimishwa sare kwenye mchezo wa kwanza
Aidha, KMC imekuwa timu ya kwanza kufunga idadi kubwa ya mabao katika mechi hizi za mwanzo msimu huu
Wana Kinondoni hao wamekaa kileleni mwa msimamo wa ligi ingawa mambo yanaweza kubadilika kutegemeana na mechi za raundi ya kwanza zilizobaki
Kagera Sugar wanacheza na JKT Tanzania kisha kufuatiwa na mchezo kati ya Azam Fc dhidi ya Polisi Tanzania
ADVERTISE HERE