Idadi kubwa ya mashabiki walijitokeza kwa wingi jana kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia mchezo wa kwanza ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2020-21, kati ya Yanga dhidi ya Tanzania Prisons
Kwa haraka haraka tu unaweza kuwa mchezo wa kwanza ambao sio wa watani wa jadi kujaza idadi kubwa ya mashabiki katika misimu ya hivi karibuni
Juhudi zilizofanywa na uongozi wa Yanga kwa kushirikiana na wadhamini GSM hasa kwenye eneo la usajili, zimewarudisha mashabiki uwanjani




Jambo muhimu sasa, timu inapaswa kuendeleza wimbi la matokeo mazuri ili mashabiki waendelee kujitokeza kwa wingi uwanjani kuiongezea timu mapato
Lakini pia, uwepo wa mashabiki wengi uwanjani unawaongezea wachezaji ari ya kupambana
Ni mwanzo mzuri, bila shaka shangwe litaendelea hivi mpaka mwishoni mwa msimu