Hii hapa sababu ya Mukoko, Kisinda kuanzia benchi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Sep 2020
Hii hapa sababu ya Mukoko, Kisinda kuanzia benchi

Jana mashabiki wa Yanga hawakuwa na furaha pale walipoona kikosi kinachoanza hakina wachezaji nyota Wacongomani Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe

Hata hivyo imefahamika kuchelewa kwa ITC za nyota hao ndio sababu iliyopelekea wasiwe sehemu ya kikosi kilichoanza kwa kuwa hawakuwa kwenye mpango wa mchezo huo

Wakati Yanga ikijiandaa na mchezo dhidi ya Prisons, ITC za nyota hao hazikuwa zimefika hivyo kwa kiasi kikubwa benchi la ufundi hawakuwa na uhakika kama wangeweza kuwatumia na kupelekea waondolewe kwenye mpango wa mchezo huo

Lakini saa chache kabla ya kuivaa Prisons, Yanga ikapokea ITC zao na wakati huo tayari kocha Zlatko Krmpotic ameshaiandaa timu yake kwa ajili ya mchezo huo uliomalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1

Bila shaka Mukoko na Tuisila watakuwa sehemu ya kikosi kitakachoivaa Mbeya City Jumapili ijayo baada ya changamoto hiyo kumalizika

Katika dakika chache walizocheza kwenye mchezo wa jana, Tuisila na Mukoko walionyesha umuhimu wao, Kisinda akipoteza nafasi kadhaa za kufunga huku Mukoko akibadili taswira ya mchezo kwa pasi zake ndefu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’