Kocha Mkuu wa Yanga Zlatko Krmpotic amesema ameyapokea matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons, anakiandaa kikosi chake kwa ajili ya mchezo unaofuata
Mserbia huyo amesema pamoja na kuwa vijana wake hawako 'fit' kwa asilimia 100, anaamini walikosa bahati kushinda mchezo huo
"Wachezaji wangu hawakuwa sawa kimwili kucheza dakika zote tisini za mchezo lakini nimeridhishwa na kile walichofanya"
"Tulikuwa na mchezo mzuri kwenye kipindi cha kwanza na hata cha pili, tulifanya mabadiliko ya baadhi ya wachezaji. Kuna muda unahitaji bahati ili ushinde, " alisema Krmpotic baada ya mchezo
Kama washambuliaji wa Yanga wangekuwa makini, wangeweza kuondoka na ushindi mnono, kosakosa zilikuwa nyingi
Nahodha Deus Kaseke alikosa nafasi ya wazi kwenye kipindi cha kwanza huku Tuisila Kisinda aliyeingia kipindi cha pili nae akikosa nafasi mbili
Mburkinabe Yacouba Songne nae akakosa nafasi nyingine wakati mchezo huo ukielekea ukingoni
Aidha akizungumzia mabadiliko ya kikosi chake akiwaacha baadhi ya wachezaji nje akiwemo kiungo Carlinhos, Krmpotic amesema alianza na wachezaji ambao walionyesha kuwa tayari kwa ajili ya mchezo huo
"Carlinhos hatukumtumia kwa kuwa bado hayuko fit. Hajafanya mazoezi ya timu kwa muda mrefu, wakati wake utafika atacheza"