Mshambuliaji wa Yanga Michael Sarpong amesema matokeo ya sare ya bao 1-1 waliyopata dhidi ya Tanzania Prisons, yamewapa machungu ya kupambana kuhakikisha mchezo unaofuata wanashinda
Sarpong alifungua akaunti ya mabao ligi kuu msimu huu jana akiisawazishia Yanga bao kwenye dakika ya 19
"Ni bahati mbaya hatukuweza kupambana kupata ushindi lakini matokeo haya yatatufanya tujiimarishe zaidi kwani huwezi kuwa imara bila kukutana na changamoto. Tunajiandaa na mchezo unaofuata," alisema Sarpong

Yanga itarejea uwanja wa Benjamin Mkapa Jumapili ijayo, Septemba 13 kuumana na Mbeya City
ADVERTISE HERE