FT : Yanga 1-1 Prisons

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Sep 2020
FT : Yanga 1-1 Prisons

Mchezo wa kwanza ligi kuu ya Vodacom msimu huu 2020/21 kati ya Yanga dhidi ya Tanzania Prisons ambao umepigwa uwanja wa Mkapa, umemalizika kwa sare ya bao 1-1

Bao la mapema walilopata Tanzania Prisons kupitia kwa Lambert Sabiyanka lilivuruga mpango wa mchezo wa mabingwa hao wa kihistoria ambao hata hivyo walirejea mchezoni kwenye dakika ya 19 kupitia kwa Michael Sarpong

Ulikuwa mchezo ambao Yanga watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kuibuka na ushindi kutokana na idadi ya nafasi walizotengeneza

Aidha ni kama kocha Zlatko Krmpotic alipiga mahesabu yake vibaya kwani kikosi alichoanza nacho kililalamikiwa na mashabiki ambapo wakati wa mapumziko alilazimika kuwaingiza Tuisila Kisinda na Yacouba Songne kuchukua nafasi ya Deus Kaseke na Farid Mussa

Kuingia kwa Kisinda kuliongeza kasi ya mashambulizi ya Yanga ambapo winga huyo mwenye kasi alikosa nafasi mbili za wazi

Pamoja na kukosa ushindi leo, kikosi cha Yanga kimeonyesha utofauti mkubwa katika uchezaji wake, lipo jambo mashabiki watalishuhudia msimu huu kutoka kwa Yanga

Kwani licha ya wachezaji kuwa na muda mchache na kocha Krmpotic, lakini timu inaonyesha kuimarika wakicheza kandanda safi linaloeleweka

Hii ni Yanga tofauti kabisa, kandanda safi inaonekana, kazi iliyobaki ni kwa benchi la ufundi kuhakikisha wanapata kikosi cha ushindi mapema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’