Mchezo wa ligi kuu ya Vodacom kati ya Yanga dhidi ya Prisons unapigwa kesho Jumamosi kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam.
Viingilio vya mchezo huo Jukwaa la VIP ni Ths 10,000/- wakati Jukwaa la kawaida ni Tsh 5,000/-
Mchezo unatarajiwa kuanza saa kumi kamili jioni.
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema Yanga itafanya mazoezi ya jioni kwenye uwanja huo unaomilikiwa na klabu ya Azam FC.
Amesema inatarajiwa kuwa na wachezaji wake wote wa kikosi cha kwanza isipokuwa Donald Ngoma ambaye bado hajarejea kutoka Zimbabwe.
Thabani Kamusoko na Papi Tshishimbi nao watakosa mchezo huo kutokana na majeruhi yanayowakabili
Aidha Ten amethibitisha mshambuliaji Amissi Tambwe baada ya kukosekana kwa muda mrefu kutokana na majeruhi, atarejea dimbani kwa mara ya kwanza na anaweza akacheza kama itampendeza kocha George Lwandamina.
Kuhusiana na swala la Donald Ngoma, Ten amesema uongozi utazungumza wakati muafaka utakapofika.
Kuna taarifa kuwa uongozi wa Yanga ulimtaka mchezaji huyo kuhakikisha anarejea nchini leo kinyume chake huenda akakumbana na adhabu kali.

ADVERTISE HERE