Uongozi wa klabu ya Yanga umewasilisha pingamizi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakipinga Mghana Bernard Morrison kuhalalishwa kuitumikia Simba licha ya kuwa na mkataba na Yanga
Mapema wiki hii TFF ilimuidhinisha Morrison kuitumikia Simba licha ya mchezaji huyo kuonekana katika usajili wa Yanga
Leo TFF wanasikiliza mapingamizi yote yaliyowasilishwa ambapo Mkurugenzi wa Mashindano TFF Salum Madadi amesema kwa mapingamizi ambayo yatakuwa na mashiko, wachezaji husika watazuiwa kushiriki ligi mpaka masuala yao yatakapopatiwa ufumbuzi
Yanga kupitia Mwenyekiti wake Dk Mshindo Msolla wamesisitiza kumtambua Morrison kama mchezaji wao halali na ndio maana hata jina lake waliliwasilisha TFF
Aidha tayari Yanga imetinga Mahakama ya Kimataifa ya Michezo (CAS) wakipinga uamuzi uliotolewa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kuhusu uhalali wa mkataba wa Morrison na Yanga
Kamati hiyo ilimtangaza Morrison kuwa mchezaji huru ikieleza kubaini mapungufu kwenye makataba aliosaini na Yanga licha ya kuwa shauri la awali ambalo Morrison alilipeleka TFF alikuwa akikana kusaini mkataba wowote na Yanga zaidi ya ule wa miezi sita ambao ulimalizika Julai 14 2020