Mmoja wa wachezaji ambao wanaweza kuwashangaza Wanayanga msimu huu ni kiungo mshambuliaji Juma Mahadhi ambaye sasa yuko fiti baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa miaka miwili
Kiwango chake kimeendelea kuimarika, ana ari ya kuwatumikia Wanajangwani hao
Mwenyewe amesema anapambana kuhakikisha anaingia kwenye kikosi cha kwanza na muhimu zaidi ni kutoa mchango wake kwa mabingwa hao wa kihistoria kila atakapohitajika
"Namshkuru Mungu baada ya miaka miwili sasa nimerejea uwanjani nikiwa nimepona kabisa. Nawashukuru mashabiki waliokuwa wakiniombea wakisubiri urejeo wangu uwanjani. Nimerejea, nitahakikisha napambania timu yangu ili tupate matokeo chanya na hata mimi nipate nafasi ya kucheza," alisema

Mahadhi bado ni yuleyule mwenye kasi yake uwanjani, mashabiki watarajie mambo mazuri kutoka kwake