Mashabiki wa klabu ya Yanga wametakiwa kuchangamkia tiketi mapema ili kuwa sehemu ya wadau watakaokishuhudia kikosi cha Yanga siku ya Jumapili kitakapoumana na Tanzania Prisons katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2020/21
Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu, utapigwa uwanja wa Benjamini Mkapa kuanzia saa moja usiku
Viingilio vya mchezo huo, Mzunguko Shilingi 5,000, Vip B & C shilingi 10,000,Vip A Shilingi 15,000.
Vituo vilivyoanza kuuza tiketi ni Buguruni Sheli, Uwanja wa Mkapa, Dar Live Mbagala, Poa Super Market Tegeta, Marere Sports Wear na Makao Makuu ya klabu ya Yanga pale Jangwani
Aidha kwa wenye kadi za ki-elektonik wanaweza kununua tiketi kupitia kadi zao
Hii sio mechi ya kukosa, utakuwa mchezo wa kwanza kabisa msimu huu wa kikosi cha Yanga kilichosukwa upya msimu huu