Wanayanga bado wanasubiri jezi mpya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Sep 2020
Wanayanga bado wanasubiri jezi mpya

Bado uongozi wa Yanga haujaweka wazi ni lini jezi mpya za klabu hiyo zitazinduliwa

Ligi Kuu inaanza keshokutwa Jumapili, pengine Yanga itaanza msimu mpya wakitumia jezi za msimu uliopita

Afisa Msemaji na Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amewataka mashabiki wawe na subira kwani watazindua jezi hizo karibuni

Aidha Nugaz amewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi siku ya Jumapili uwanja wa Mkapa kuiunga mkono timu yao itakapokuwa ikichuana na Tanzania Prisons katika mchezo wa ufunguzi wa ligi msimu wa 2020/21

"Suala la jezi tutawatangazia Wanachama na Mashabiki wetu hivi karibuni, muhimu Jumapili tujitokeze kwa wingi tukaiunge mkono timu yetu ili kuhakikisha tunaanza msimu vizuri," alisema

Awali ilielezwa kuwa jezi hizo zingezinduliwa kabla ya wiki hii kumalizika lakini inaonekana bado ipo changamoto

Wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said alisema changamoto ya ndio iliyopelekea jezi hizo kuchelewa

Ikumbukwe huko China bado wanaendelea na lockdown kutokana na ugonjwa wa corona, hivyo mizigo inayotoka nchini humo inachelewa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’