Keshokutwa Jumapili, kikosi cha Yanga kitashuka uwanja wa Mkapa kuikabili Tanzania Prisons katika mchezo wa ufunguzi wa msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom
Safu ya ushambuliaji ya mabingwa hao wa kihistoria inatarajiwa kuongozwa na Mghana Michael Sarpong ambaye alifungua ukurasa wa mabao kwenye mchezo wa wiki ya Mwanachi

Msimu uliopita kilio cha Wanajangwani kilikuwa katika safu ya ushambuliaji, lakini msimu huu wengi wana matarajio makubwa, mambo yatakuwa tofauti
Kwani safu hiyo imesukwa upya, imesheheni wachezaji makini, wenye uzoefu wa mikikimikiki ya michuano ya Kimataifa
Pamoja na Sarpong, waangalie Tuisila Kisinda, Yacouba Songne na Farid Mussa hawa ni wachezaji ambao safu yoyote ya ulinzi haitatamani kukutana nao
Eneo la kiungo mafundi kama Zawadi Mauya, Feisal Salum, Mukoko Tonombe, Carlinhos na Haruna Niyonzima hawa watakuwa na kazi ya kuwarahisishia washambuliaji kufunga mabao
Sarpong amesema yuko nchini kwa kazi moja tu, kuifungia Yanga mabao hivyo mashabiki wasubiri mambo mazuri kutoka kwake