Waamuzi watahadharishwa VPL 2020/21

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Sep 2020
Waamuzi watahadharishwa VPL 2020/21

Bodiya Ligi Tanzania Bara (TPLB), imesema msimu ujao wa 2020/21 hawatawafumbia macho waamuzi ambao watashindwa kutafsiri sheria 17 za soka kwa maslahi binafsi.

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almas Kasongo, amesema msimu uliopita ulikuwa na malalamiko mengi kwa waamuzi.

 "Yapo  malalamiko ambayo yalifanyiwa kazi na Kamati ya Waamuzi baada ya kufika mezani, lakini mengi yalishindwa kuchukuliwa hatua kwa sababu hakukuwa na ushahidi wa kutosha"

"Bodi ambayo ina dhamana ya Ligi za Tanzania, msimu huu tutafuatilia kila mechi itakayochezwa kuanzia Daraja la Pili (SDL), Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Kuu  (VPL) na ikitokea tukabaini kuna mapungufu kwa yeyote hatutasita kuingilia kati ili kuhakikisha hatua stahiki inachukuliwa na wale watakaobainika kufanya mchezo mchafu"

"Tunahitaji ligi ya msimu huu iwe ya tofauti kubwa na zile zilizotangulia hasa katika kuhakikisha waamuzi wanatimiza wajibu wao kikamilifu kwa sababu tunaamini wao ndio chanzo cha kuharibu mchezo  mzima pale watakapofanya maamuzi kinyume na sheria 17 zilizowekwa," Kasongo amenukuliwa na gazeti la Bingwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’