Vibali vya maproo Yanga safi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Sep 2020
Vibali vya maproo Yanga safi

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa wamekamilisha taratibu za kupata vibali vya kufanya kazi nchini nyota wake wote wa kigeni hivyo wanategemea watawatumia kwenye mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa Jumapili ijayo, uwanja wa Mkapa

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wachezaji hao wataitumikia Yanga Jumapili

"Utaratibu wa kupata vibali kwa wachezaji wetu wa kigeni pamoja na benchi la ufundi umekamilika kwa asimilia kubwa. Tunategemea kuwatumia wote katika mchezo wa wetu wa kwanza wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons siku ya Jumapili," alisema Bumbuli

Jana Serikali iliviagiza vilabu vyote vilivyosajili nyota wa kigeni kuwasilisha vibali vyao Uhamiaji huku ikisisitiza kuwa hakuna timu inaruhusiwa kumtumia mchezaji wa kigeni kama hana kibali cha kufanya kazi nchini

Yanga imeongeza nyota watano wa kigeni ambao wanapaswa kukatiwa vibali hivyo

Nyota hao ni winga Tuisila Kisinda, viungo Mukoko Tonombe, Carlinhos na washambuliaji Michael Sarpong na Yacouba Songne

Pia kocha Zlatko Krmpotic nae atahitaji kuwa na kibali ili aweze kuruhusiwa kukaa kwenye benchi la mabingwa hao wa kihistoria

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7m ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
14h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
18h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
19h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
19h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’