Baada ya kukiimarisha kikosi cha wanaume, uongozi wa Yanga umegeuka upande wa Yanga Princess ambapo wanaimarisha kikosi hicho ili kuhakikisha msimu ujao mataji yote yanaelekea Mtaa wa Twiga na jangwani yalipo Makao Makuu ya mabingwa hao wa kihistoria
Jana Yanga Princess litambulisha usajili wa wachezaji wawili Tabea Munga aliyetokea Simba Queens na beki Emeliayana Mdimu aliyetokea klabu ya Mlandizi Queens
Pia mchezaji Fatma Mwisendi yeye akaongezewa mkataba kuendelea kukipiga na kinadada hao


Leo Yanga Princess imetangaza kumnasa Wincate Kaari Kinyua kutoka nchini Kenya klabu ya Thika Queens, akisaini mkataba wa mwaka mmoja

ADVERTISE HERE