Winga Mrisho Ngasa amejiunga na klabu ya Ndanda Fc ambayo msimu ujao itashiriki ligi daraja la kwanza
Baada ya kutemwa kwenye kikosi cha Yanga, Ngasa ataunga na 'swahiba' wake Gerson Tegete kuitumikia timu hiyo iliyopania kurejea ligi kuu
Ngasa ni mmoja wa wachezaji waliokuwa wakikubalika sana na mashabiki wa Yanga, na hata alipoachwa wengi walitoa maoni arejeshwe kikosini
Hata hivyo uongozi wa Yanga ulisisitiza kuwa hatua walizochukua zilikuwa muhimu katika kukiimarisha kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria
Juma Abdul na Kelvin Yondani ni wachezaji wengine ambao pia walikuwa wakikubalika sana na mashabiki lakini panga liliwapitia
Tunawatakia kila la kheri miamba hawa katika maisha yao ya soka nje ya Yanga
ADVERTISE HERE