Dirisha la usajili limefungwa usiku wa kuamkia leo huku Yanga ikisajili wachezaji 27, miongoni mwao wachezaji nane wakiwa wa kigeni
Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema wameridhika na kikosi walichonacho lakini kwenye usajili wa dirisha dogo mwezi Disemba, wataongeza wachezaji wawili ambao ni beki wa kati na mshambuliaji
Aidha Dk Msolla amewapongeza wachezaji wa Yanga kwa kuonyesha kandanda safi siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi licha ya kufanya mazoezi pamoja kwa muda mfupi
"Tumefanya usajili mzuri, timu yetu imeimarika, nadhani mmeona vijana walivyocheza vizuri jana (juzi). Kuna watu walikuwa wakisubiri tufungwe ili watucheke lakini hali imekuwa tofauti. Pamoja na wachezaji kufanya mazoezi kwa muda mfupi, wameonyesha uwezo mzuri," alisema Dk Msolla
"Dirisha la usajili lmefungwa, sasa tunaelekeza nguvu zetu kwenye ligi. Dirisha dogo tunaweza tukaongeza wachezaji wawili ili kukiimarisa kikosi zaidi. Tumeona ipo haja ya kuongeza beki mmoja wa kati pamoja na mshambuliaji"
Yanga ilikamilisha usajili wake jana kwa kumpa mkataba wa miaka miwili mshambuliaji Yacouba Songne aliyetua kutoka Burkina Faso
Songne alikuwa akiitumikia klabu ya Asante Kotoko ya nchini Ghana