Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Tariq Seif Kiakala amejiunga na Polisi Tanzania kwa mkataba wa miaka miwili
Tariq alitua Yanga kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari 2020 akitokea nchini Misri alikokuwa akicheza soka la kulipwa
Hakuwa na wakati mzuri kwenye kikosi cha Yanga, mabingwa hao wa kihistoria wakiamua kuachana nae baada ya mkataba wake wa miezi sita kumalizika
Nyota huyo alitua Polisi Tanzania muda mchache kabla ya dirisha la usajili kufungwa usiku wa kuamkia leo
Kila la kheri mwamba...!
ADVERTISE HERE