Dirisha la Usajili kuelekea msimu wa 2020/21 linafungwa leo saa 5:59 usiku, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limevitaka vilabu kuhakikisha wanakamilisha usajili wao katika muda uliobaki kwani hakutatolewa muda zaidi
Kwa Yanga ni kama ilishafunga hesabu zake mapema, ikiunda kikosi cha wachezaji 27 lakini bado wana nafasi moja ya nyota wa kigeni ukiondoa ile ya Morrison ambaye jana alitambulishwa kuwa mchezaji halali wa Yanga
Inaelezwa kocha mkuu wa Yanga Zlatko Krmpotic ambaye jana alikishuhudia kikosi chake kwa mara ya kwanza, anaweza kupendekeza nafasi hiyo ijazwe ingawa Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla alisema wanaweza kuitumia kwenye dirisha dogo la usajili
ADVERTISE HERE