Huu ni usajili wa maana sana Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Aug 2020
Huu ni usajili wa maana sana Yanga

1. Tuisila Kisinda

Kisinda amesajiliwa na Yanga akitokea klabu ya AS Vita, amefanya mazoezi kwa takribani siku tano tu na kikosi cha Yanga

Hii ni mashine kwelikweli, ana kasi na akili, anakimbiza na akipata nafasi anajaribu. Kwa huyu wapinzani watakuwa na wakati mgumu kumdhibiti

2. Mukoko Tonombe

Huyu ni kiungo mkabaji halisi. Yuko eneo lake la kazi muda wote. Anazuia, anachezesha timu na pale anapopata nafasi ya kushambulia hapotezi muda

Huu ni usajili mwingine ambao Wanayanga wataufurahia msimu huu

3. Farid Mussa

Dakika zake alizocheza kwenye kipindi cha pili zimeonyesha Farid ni mchezaji atakayekuwa na faida sana kwa Yanga

Ana kasi, nguvu na akili. Farid sio muoga, ni aina ya wachezaji ambao walinzi wengi hawatamani kukutana nao

Sijui itakuwaje pale watakapoanza pamoja na Kisinda. Kasi yao itakuwa shida kwa timu pinzani

4. Zawadi Mauya

Katika eneo ambao kocha wa Yanga atapta shida kupanga ni eneo la kiungo

Mauya aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mukoko. Kazi aliyokuwa akiifanya Mukoko naye aliifanya kwa ustadi

Mauya hakuja Yanga kwa bahati mbaya, ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa na hilo ameanza kulithibitisha mapema

5. Kibwana Shomari

Anazuia timu inaposhambuliwa na pia ni mwepesi kupanda kuongeza mashambulizi. Krosi zake zinanikumbusha enzi za Juma Abdul

Ana kasi na mara nyingi yuko eneo analopaswa kuwepo

6. Yassin Mustafa

Katika mchezo dhidi ya Aigle Noir, upande anaocheza ulitumika sana kwenye kupanga mashambulizi

Yassin alikuwa na uelewano mzuri sana na Tuisila Kisinda. Kazi yake imeonekana uwanjani leo, hakuna shaka ubora wake utaendelea kuonekana kadiri atakavyokuwa akipewa nafasi

7. Michael Sarpong

Amefunga bao na kufanya majaribio kadhaa katika mchezo wake wa kwanza. Hiyo ndio sifa ya mshambuliaji. Tangu atue Yanga amefanya mazoezi chini ya siku tano

Hakuna shaka, Sarpong atafunga mabao mengi katika kikosi cha Yanga

8. Waziri Junior

Ni mchezaji aliyeonyesha kuwa na vitu vingi mguuni. Leo alikuwa na papara kwa kuwa alikuwa na shauku kubwa ya kufunga. Lakini ameonyesha ni mshambuliaji msumbufu, Wanayanga watarajie mambo mazuri kutoka kwake

9. Carlinhos

Alicheza kwa takribani dakika nane tu, lakini alifanya jaribio moja ambalo nusura lizae bao. Kiungo huyo ni kawaida yake kupiga mashuti ya mbali

Amechelewa kujiunga na Yanga, amefanya mazoezi kwa siku tatu tu, lakini huyu mpira anaujua

10. Bakari Mwamnyeto

Ni yuleyule ambaye mashabiki walikuwa walimtarajia. Leo amecheza vizuri sana akishirikiana na Abdallah Shaibu Ninja

Bado ni mapema lakini ni wazi ni mchezaji ambaye atakuwa nguzo muhimu kwenye safu ya ulinzi Yanga

11. Abdallah Shaibu 'Ninja'

Amerejea kutoka kule Marekani alikoitumikia LA Galaxy kwa takribani miezi sita

Ni mchezaji anayeonyesha kupevuka zaidi, sasa akicheza kama mchezaji kiongozi

Kwa hakika safu ya ulinzi ya Yanga msimu huu ina watu..!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’