Kocha Mkuu wa Yanga Zlatko Krmpotic ni kocha mwenye uzoefu mkubwa, akipata mafanikio tangu wakati akiwa mchezaji wa timu ya Taifa ya Yugoslavia
Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amesema hawakukurupuka katika uteuzi wake, wanaamini ni kocha sahihi kujiunga na Yanga wakati huu baada ya kumkosa Cedric Kaze aliyepata matatizo ya kifamilia dakika za mwisho
Wasifu wa Krmpotic
KUZALIWA: 7 AUGUST 1958
ALIPOCHEZA: 1977-1986 Red star Belgrade (mechi 180 magoli 7) akiwa beki.
1986-1988 Genclerbirling
TIMU YA TAIFA
Yugoslavia U21 mechi 5 (1978)
Yugoslavia wakubwa (1980-82)
UKOCHA
1994-96 Degerfors IF
97-98 Sloga Jugomagnat
99-20 OFK Beograd/Obilic
2001- Pamiliakos/Nea Salamis
2002- Kairat
2005- Serbia & Montenegro U17
2006- Kazma
2007-8 Serbia U19
2013- OFK Beograd
2015- TP Mazembe (msaidizi)DRC
2016- Don Bosco (DRC)
2017- Zesco United (Zambia)
2018- Jwaneng Galaxy
2019- APR (Rwanda)
2019- Polokwane city (SA)
Akiwa kocha mafanikio makubwa aliyopata hapa Afrika ni pamoja na ubingwa wa Afrika (Ligi ya Mabingwa)Β mwaka 2015 wakati akiwa kicha msaidizi wa TP Mazembe
Lakini mwaka 2017 aliiwezesha Zesco United kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Zambia. Alichukua nafasi ya George Lwandamina ambaye alikuja nchini kujiunga na Yanga
Krmpotic anatarajiwa kuwasili nchini kesho Jumamosi, amepewa mkataba wa miaka miwili na atasaidiwa na Juma Mwambusi ambaye tayari amenza majukumu yake ndani ya Yanga