Tumekamilisha ahadi tulizotoa Yanga - Injinia Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Aug 2020
Tumekamilisha ahadi tulizotoa Yanga - Injinia Hersi

Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amesema ahadi walizotoa kwa Wanayanga kuelekea msimu mpya wamezikamilisha kwa asilimia 95

Aidha katika majojiano na Wasafi Radio mapema leo, Injinia Hersi alibainisha mambo kadhaa ambayo wameyafanya na wanayokusudia kuyafanya msimu huu;

βœ”Mwaka huu ni mwaka wa mabadiliko kwa klabu yetu ya Yanga, na tutafanya makubwa sana kimafanikio kama tulivyoahidi sisi GSM.

βœ”Gumu zaidi ilikuwa usajili wa Mwamnyeto ambaye wenzetu walishamtaja kama mchezaji wao lakini kuonesha tupo serious tulifanikisha kumchukua.

βœ”Lengo letu ilikuwa kujenga kikosi chetu, kiwe imara na kutupata matokeo. .kama wadhamini tumefanikiwa kwa asilimia kubwa sana.

βœ”Kama mdhamini hatuwezi kuwa katika klabu ambayo haiwezinkutupa matokeo, mwaka jana tulifanya kwa mapenzi yetu, lakin sasa tunafanya kwa dhana ya uwajibikaji.

βœ”Nimekuwa nafanya majukumu mengi ambayo sio taaluma yangu ndio maana tumemuajiri Senzo Mbatha mtaalamu wa haya mambo ili sisi tukae pembeni kama wadhamini.

βœ”Tumefanya analysis ya kutosha kabla ya usajili, tumefanya usajili kucover udhaifu wa kikosi chetu, Makipa tunao wazuri sana Metacha na Shirkalo wapo national team hapa ina maana tuna makipa bora sana lakini walikosa mafunzo sahihi ndio maana tumemleta kocha wa makipa bora kutoka Burundi.

βœ”Beki ya kulia, kuna Kibwana Shomari, na kushoto yupo Yussuf katikati Mwamnyeto, baada ya kumpoteza Tshishimbi tumemleta mchezaji wa timu ya Taifa Congo huyu ni Top Player Tonombe Mukoko, kulia kuna mchezaji matata sana Tuisila Kisinda kushoto yupo Farid Mussa na wengineo matata sana.

βœ” Kelvin Yondani na Juma Abdul hawana nafasi tena, maana tulishafunga usajili wa wachezaji wa ndani pia hakuna ukweli wowote kuhusu kumsajili Jack Tuisenge!

βœ”Tuna vikosi viwili, cha ndani ambacho hakimhitaji mgeni hata mmoja. . Metacha, Shomari, Yussuf, Ninja, Mwamnyeto, Zawadi Mauya, Kaseke, Feitoto, Waziri, Balama, Nchimbi.

βœ”Kuna aina 3 za umiliki, tupo katika hatua za kuchambua kila aina ya umiliki na faida zake ili kucomply na agizo la serikali kuwa 51% wanachama na 49 % mwekezaji.

βœ”Senzo atakuwa mshauri wa utendaji wa klabu yetu, anakuja kufanya ushauri katika operation team. . atasimamia mikataba ya wachezaji na wafanyakazi, pia budget ya kuendesha klabu kisasa zaidi. .

βœ”Senzo atasimamia mishahara, vyanzo vya mapato kusimamia na kuongeza na pia na mambo mengine ya kiutawala.

βœ”Tumeshare organogram na Senzo tumempa nafasi yeye apendekeze leadership structure ya klabu yetu.

βœ”Baada ya siku ya wananchi Senzo atakuwa busy sana kuandaa set up nzima ya klabu yetu huku tukisubiri maelekezo kutoka La Liga.

βœ”Senzo ana mkataba wa mwaka mmoja and there is a room for extension.

βœ”Jezi tutazindua rasmi na tutatoa utaratibu kupitia klabu yetu, jezi hii ina uzuri kuzidi mipaka. Jezi inakuja na concept yenye feature na uhalisia wa klabu yetu. .kuna changamoto ya kontena kuchelewa lakini mzigo utafika mapema na kutosheleza nchi zima.

βœ”Tuna jezi tatu, ya nyumbani ,ugenini na third kit. .

βœ”Kisinda na Mukoko ni wachezaji wakubwa , Mukoko anamilikiwa na As Vita , Tuisila anamilikiwa na Union Manyema alikuwa Vita kwa Mkopo. . usajili huu ndio ulinipa changamoto kubwa sana! tulivunja mikataba yao pia tuliwapa signing fees!

βœ”Congo passport za wachezaji humilikiwa na vilabu, baada ya kuzipata tulipofika airport wachezaji walitakiwa kuwa authorised na klabu hivyo tukasubiri dk 45.

βœ” Kuna watu walienda Ethiopia kumpokea Carlinhos, lakini hawakujua utaratibu wa Ethiopia. . ndugu zetu wa Simba SC walipoenda Ethiopia waliwekwa karantini kwa maana Ethiopia ipo karantini! walimpigia simu aliwaambia pesa haiwezi kumnunua yeye anaenda Yanga SC.

βœ”Most expensive city in Africa ni Luanda Angola, Carlinhos ni mchezaji mwenye uwezo kifedha na amekuja Yanga SC kwa mapenzi yake mwenyewe,watu wamejaribu kuichafua klabu yetu ili asije lakini alishikilia msimamo Angola pia wameshangaa kwa kipaji chake atakujaje Tanzania?

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
37m ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
15h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
19h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
20h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
20h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’