Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amemtangaza Zlatko Krmpotic raia wa Serbia kuwa kocha mkuu wa Yanga, mabingwa wa kihistoria
Injinia Hersi amemtangaza kocha huyo katika mahojiano na kipindi cha michezo cha Wasafi FM, mapema leo
Zlatko alikuwa akiinoa klabu ya Polokwane City inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini
Amepewa mkataba wa miaka miwili, anatarajiwa kuwasili siku ya kesho Jumamosi
Zlatko ni kocha mwenye uzoefu na soka la Afrika akizinoa klabu za Zesco United, APR na TP Mazembe ambayo mwaka 2015 ilitwaa ubingwa wa Afrika yeye akiwa kocha msaidizi
ADVERTISE HERE