Kutowasili kwa kocha Cedric Kaze ni kama kumevuruga mipango ya Yanga ambayo ilikuwa tayari imefunga mahesabu nafasi ya Kocha Mkuu
Hata hivyo uamuzi wa kumchukua kocha Juma Mwambusi wakati huu unaweza kuwa sahihi kwani kwa muda uliobaki kuelekea msimu mpya, kuanza na kocha mgeni wa ligi ya Tanzania inaweza kuwa changamoto
Mwambusi anatarajiwa kuiongoza Yanga katika mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi siku ya Jumapili dhidi ya Aigle Noir na pengine hata mechi za mwanzo msimu huu
Huyu ni kocha anayeifahamu vizuri Yanga, misimu mitatu aliyokuwa na makocha Hans van Plkuijm na baadae George Lwandamina, inamfanya kuwa chaguo sahihi kwa nyakazi hizi za dharura
Wanachopaswa kufanya Wanayanga ni kumuunga mkono ili aweze anatimiza majukumu yake vyema
Mashabiki tumekuwa na kawaida ya kuwapuuza makocha wetu wazawa licha ya ukweli kuwa wakiaminiwa wanaweza kufanya mambo makubwa
Β Mwambusi amepewa mkataba wa miaka miwili, hivyo hata atakapokuja kocha mkuu, ataendelea kuhudumu kama kocha msaidizi