Upo uwezekano mkubwa Hans van Pluijm kocha wa zamani wa Yanga aliyepata mafanikio zaidi katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, huenda atakabidhiwa kibarua cha kuwanoa mabingwa hao wa kihistoria
Yanga tayari imemteua kocha Juma Mwambusi kusimamia mazoezi wakati huu wakisubiri kutangaza kocha mkuu
Lakini ni wazi huenda tayari wamemalizana na Pluijm na pengine ujio wa Mwambusi ni pendekezo lake
Pluijm na Mwambusi walifanya kazi pamoja kwenye kikosi cha Yanga kilichokuwa moto wa kuotea mbali kilichotwaa ubingwa kwa misimu miwili 2014/15 na 2015/16 na mwanzoni mwa msimu uliopita walikuwa pamoja kule Azam Fc
Kutokana na ufinyu wa muda, Yanga imelazimika kutafuta kocha mwenye uzoefu na soka la Tanzania, kocha ambaye tayari anafahamu ni kitu gani anapaswa kufanya katika muda uliopo
Jana uongozi wa Yanga ulibainisha kuwa wakati wowote watamtangaza kocha mkuu