Juma Mwambusi aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Yanga wakati wa Hans Van Pluijm, leo alihudhuria mazoezi ya Yanga uwanja wa Chuo cha Sheria, Mawasiliano jijini Dar es salaam akitarajiwa kukabidhiwa mikoba ya kocha msaidizi
Mwambusi aliwashuhudia vijana wa Yanga wakicheza mechi ya kirafiki dhidi ya African Sport mapema leo na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1
Bado mabingwa hao wa kihistoria wanasubiri ujio wa kocha mkuu Cedric Kaze huku kukiwa na taarifa kuwa anaweza kuteuliwa kocha mwingine baada ya Kaze kutoa taarifa anaweza kuchelewa zaidi, anakabiliwa na matatizo ya kifamilia
ADVERTISE HERE