Kiungo fundi wa Yanga Mapinduzi Balama afya yake imezidi kuimarika akitarajiwa kurejea uwanjani baada ya majuma manne
Balama alipata majeraha ya kifundo cha mguu kwenye maandalizi ya mwisho ya kumalizia msimu uliopita
Mchezaji huyo amekuwa chini ya uangalizi makini wa Madaktari wa Yanga kukiwa na matumaini kuwa anaweza kurejea kuwanjani mwishoni mwa mwezi wa tisa
Kaimu kocha mkuu wa Yanga Riedoh Berdien ambaye ni mtaalamu wa viungo, amesema Balama anaendelea na program maalum ya mazoezi
"Balama anaendelea na programu yake kwa sasa kwani baada ya kupata majeraha msimu uliopita, alikuwa chini ya uangalizi wa jopo la wataalamu ambao wapo naye mpaka sasa.
"Kwa sasa anaendelea vizuri kwa mujibu wa ripoti na anaweza kuanza kuwa na wenzake baada ya wiki nne ama tatu, itategemea na ripoti kutoka kwa madaktari," amesema Berdien