Tutamaliza usajili tuliopanga - Injinia Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Aug 2020
Tutamaliza usajili tuliopanga - Injinia Hersi

Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Yanga amesema, GSM watakamilisha michakato yote ya usajili kama ilivyopangwa

Jana Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla aliwataka wanachama na wadau wote wa Yanga wachangie usajili wa nyota wawili wa kigeni

Aidha Dk Msolla akafafanua kauli hiyo kuwa alimaanisha wachezaji wapya nje ya hawa ambao tayari michakao yao ya usajili imekamilika

Injinia Hersi amesema wameisikia kauli ya Mwenyekiti lakini wanaamini ni maoni yake, kwani kwa upande wao wamejipanga kukamilisha michakato yote ya usajili

Hersi amewataka Wanayanga siku ya kesho Jumanne, wajitokeze kwa wingi uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wampokee kiungo kutoka Angola, Carlinhos

Aidha kuhusu ujio wa kocha, Mhandisi Hersi amesema Kaze ataondoka nchini Canada siku ya keshokutwa Jumatano, atatua nchini siku ya Ijumaa

"Nimeisikia kauli ya Mwenyekiti, labda ni mawazo yake lakini nawahakikishieni sisi GSM tupo imara kabisa kumalizia usajili tulioupanga"

"Kesho nawakaribisha Uwanja wa kimataifa wa JK kumpokea kiungo bora zaidi kushuka katika ardhi ya Tanzania"

"Kuhusu Mwalimu Kaze anatua siku ya Ijumaa akitokea Canada, ambapo ataondoka Canada keshokutwa Jumatano," amesema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
54m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’