Jana Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dk Mshindo Msolla aliwataka wapenzi, wanachama na mashabiki kuchangia fedha ili kukamilisha usajili wa wachezaji wawili kutoka nje ya nchi
Hata hivyo baadhi ya wadau wameipokea tofauti kauli hiyo ya Dk Msolla wengine wakidai anawavunja moyo mashabiki
Yanga ni timu ya Wananchi, kila mmoja anafahamu mchakato wa Mabadiliko ndio uko kwenye hatua za awali, awamu ya kwanza ikitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu
Mpaka sasa, usajili unaofanywa na GSM ni wa kujitolea, wenyewe mara kadhaa wamelieleza hili kuwa, jambo hili liko nje ya mkataba, wanalifanya kutokana na mapenzi yao kwa Yanga
GSM wamefanya kazi kubwa ya kusajili wachezaji bora na wenye hadhi, Wanayanga wanaweza kutoa mchango wao kwa kushiriki kukamilisha usajili wa wachezaji wawili
Ikumbukwe awali Yanga ilitangaza kuwa ingesajili nyota nane tu wa kigeni, lakini sasa imeonekana umuhimu wa kuongeza wachezaji hao wawili. Na haya ni mapendekezo ya wadau waliowengi kuwa ni vyema nafasi zote za kigeni zikajazwa ili kuwa na kikosi kipana zaidi
Kumhukumu Mwenyekiti Dk Msolla kwa kauli yake sidhani kama ni kumtendea haki kwani alichofanya yeye ni kuwashirikisha Wanachama na Mashabiki kwani wao ndio wenye timu
Msimu uliopita Wanayanga walishiriki kwa asilimia 90 kwenye usajili, hawawezi kushindwa kwa hawa wawili
Hili ni jambo la kawaida sana kwa timu ya Wananchi, wanaolikuza ni wale wanaotaka ionekane kuwa Yanga hakuna hatua yoyote waliyopiga licha ya jitihada kubwa zinazofanywa na viongozi wakishirikiana na wadhamini wao SportPesa, Taifa Gas na GSM ambao ni Wahisani pia