Mashabiki Yanga wampagawisha Sarpong

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Aug 2020
Mashabiki Yanga wampagawisha Sarpong

Mshambuliaji mpya wa Yanga Michael Sarpong ameeleza furaha yake baada ya kukamilisha usajili na mabingwa hao wa kihistoria

Sarpong (24) alisaini mkataba wa miaka miwili jana ambao utamfanya abakie Jangwani mpaka mwaka 2022

Ujio wa Mghana huyo aliyeitumikia Rayon Sports msimu uliopita, ulikuwa kama tetesi lakini baada ya kutua mwenyewe ameeleza kushitushwa na mapokezi aliyopata

"Tangu nilipokuwa Kumasi (Ghana) nilikuwa nikiona shamrashamra zilizokuwa zikiendelea hapa. Sikuwahi kushuhudia tukio la kupokewa na idadi ile ya mashabiki uwanja wa ndege, hii ni mara yangu ya kwanza"

"Nimekuja hapa kufanya kazi, tuna malengo makubwa msimu huu, kwa ushirikiano wetu pamoja na usaidizi wa Mungu tutaweza kufanikiwa," alisema Sarpong

Sarpong alikuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Rwanda msimu wa 2018/19 akifunga mabao 16 akiwa na klabu klabu ya Rayon

Msimu wa 2019/20 alifunga mabao nane, hata hivyo alicheza nusu ya msimu tu baada ya kutokea sintofahamu baina yake na uongozi wa Rayon na hivyo kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake

Ametua Yanga akiwa mchezaji huru akiungana na nyota wengine wa kigeni waliosajilwa, Yacouba Sogne, Tonombe Mukoko, Tuisila Kisinda, na Carlinhos

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14m ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
22m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
3h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
22h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’