Uongozi wa klabu ya Yanga umethibitisha kumalizana na kocha raia wa Burundi Cedric Kaze
Akizungumza mapema leo kwenye uzinduzi wa Wiki ya Mwananchi uliofanyika mkoani Dodoma, Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindi Msolla amesema Kaze amesaini mkataba wa miaka miwili kuwanoa mabingwa hao wa kihistoria
"Klabu yetu imeingia mkataba wa miaka miwili na kocha Kutoka Burundi,Cedric Kaze aliyekuwa anafundisha Academy ya Barcelona nchini Canada na Kaze anatarajia kuwasili Tanzania wiki ijayo," alisema
Pamoja na kuwa bado hajawasili nchini akisubiri kukamilika kwa taratibu za vipimo vya corona, inaelezwa kocha huyo mwenye uzoefu mkubwa, ndiye anayeandaa program za mazoezi ys Yanga yanayosimamiwa na kocha msaidizi, mtaalamu wa viungo Riedoh Berdien
ADVERTISE HERE