Mchana wa leo Ijumaa, Wanayanga walikuwa pale uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kumpokea mshambuliaji mpya wa timu hiyo Michael Sarpong
Sarpong alipokelewa na Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM, Mhandisi Heri Said ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano
Ujio wake unafunga hesabu kwenye safu ya ushambuliaji kwani katika nafasi hiyo ataungana na Mburkinabe Yacouba Soghne na wazawa Waziri Jr na Ditram Nchimbi
Sasa wanasubiriwa wachezaji wawili Yacouba na Carinhos Carmo 'KDB', Kiungo mshambuliaji ambaye anasubiri majibu yake ya corona kabla ya kuruhusiwa kusafiri kutoka Angola
Nyota hao wanatarajiwa kuwasili wikiendi hii




ADVERTISE HERE