Mshambuliaji Michael Sarpong raia wa Ghana tayari ametua nchini kujiunga na mabingwa wa kihistoria, Yanga
Sarpong amewasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere mchana wa leo akitokea nchini Norway alikokuwa mapumziko
Anakuwa mchezaji wa nne wa kigeni kusajiliwa na Yanga dirisha hili la usajili
Wengine waliosajiliwa ni Tuisila Kisinda, Mukoko Tonombe na Yacouba Sogne
Pia yumo kiungo kutoka Angola, Carlinhos anayesubiriwa kutua mwishoni mwa wiki

Hakika, Wananchi wakiwa na jambo lao hawashindwi...!
ADVERTISE HERE