Wakati ligi kuu ya Vodacom ikiingia mzunguuko wa 11 wikiendi ijayo, Obrey Chirwa ameyarejesha makali yake ya upachikaji mabao.
Mabao yake matatu aliyofunga dhidi ya Mbeya City yamemfanya afikishe mabao sita na kushika nafasi ya pili akiwa amefungana na Mohammed Rashid wa Prisons.
Chirwa anahitaji mabao mawili tu kumfikia mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi ambaye ndiye kinara wa mabao ligi kuu ya Vodacom akiwa na mabao nane.
Huu ni wakati mwafaka kwa Yanga kuanza jitihada za kumuongeza mkataba mkali huyo raia wa Zambia ambaye ndio kwanza ana umri wa miaka 23.
Mkataba wa Chirwa kuitumikia Yanga unamalizika Juni 30, 2018 kuanzia mwezi ujao atakuwa huru kufanya mazungumzo na timu yoyote kwa kuwa mkataba wake utakuwa chini ya miezi sita.
Halitakuwa jambo jema kuacha mkataba wake ufike mwisho, hatari ya kumpoteza itakuwa kubwa.

ADVERTISE HERE