Mashabiki maarufu wa klabu ya Yanga Akili Jr na Sekeli wao wamelala hapo JNIA wakisubiri ujio wa nyota wapya wa Yanga waliosajiliwa kutoka klabu ya AS Vita Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe
Mashabiki hao walitua JNIA jana jioni na wametimiza ahadi waliyoweka kwa kulala uwanjani hapo wakiwa tayari kuwapokea nyota hao
Tuisila na Mukoko watatua majira ya saa saba mchana wakiongozana na Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Yanga, Mhandisi Hersi Said
Utambulisho rasmi wa nyota hao pamoja na wengine waliosajiliwa wiki hii, unatarajiwa kufanyika kwenye tukio la ufunguzi wa Wiki ya Mwananchi ambalo litafanyika mkoani Dodoma siku ya Jumamosi, August 22 2020
ADVERTISE HERE