Wachezaji kutoka DR Congo Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe watawasili kesho Alhamisi mchana wakiongozana na Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said
Taarifa zilizopatikana mapema leo, zilibainisha kuwa nyota hao wote tayari wameondoka DR Congo, Tuisila akitangulia na Mukoko akafuatia
Msemaji na Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz, ameeleza kuwa nyota hao watafika pamoja wakiongozana na Injinia Hersi
"Kesho Alhamis saa saba kamili mchana ndani Mwalimu Nyerere International Airport ndio siku ambayo Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe na Injinia Hersi Said wanatua kwenye ardhi ya Tanzania"
"Naomba wanachama,wapenzi na Mashabiki kwa upendo wetu tujitokeze kuwapokea ili wajue Kuwa wamekuja kwenye timu ya Wananchi kwa kuwapa mapokezi ya hali ya juu"
"Tukutane pale. Vyuma viwili vipo njiani navyo"