Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amesema baada ya kukamilisha taratibu za usajili wa wachezaji Tonombe Mukoko na Tuisila Kisinda, atatua nchini na wachezaji hao siku ya Alhamisi mchana
Injinia Hersi yuko DR Congo tangu juzi ambako amefanikiwa kukamilisha usajili wa wachezaji hao wanaosubiriwa kwa hamu na Wanayanga
"Tunashukuru tumekamilisha salama taratibu zote za usajili, kwa sasa tunashughulikia vibali vyao tuweze kusafiri nao, Mungu akitujaalia Alhamisi mchana tutawasili huko nyumbani," alisema Injinia
Mukoko, Kisila pamoja na nyota wengine wapya, wanatarajiwa kukaribishwa rasmi ndani ya Yanga siku ya ufunguzi wa Wiki ya Mwananchi, tukio la kihistoria ambalo litafanyika mkoani Dodoma, Jumamosi August 22 2020
ADVERTISE HERE