Niyonzima apongeza usajili Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Aug 2020
Niyonzima apongeza usajili Yanga

Kiungo fundi wa Yanga Haruna Niyonzima ameeleza kufurahishwa na usajili unaofanywa na mabingwa hao wa kihistoria akiamini unakwenda kumaliza changamoto walizokuwa nazo msimu uliopita

Niyonzima amesema amefuatilia usajili huo kwa makini na amejiridhisha kuwa umezingatia kumaliza mapungufu yaliyokuwepo kiufundi

"Nafurahishwa na usajili unaoendelea ndani ya timu yangu . Ni usajili unaozingatia mapungufu yetu kimbinu na kiufundi pia kuipa timu nguvu ya kupambana kwa maana ya kutazama aina ya wapinzani wetu na malengo yetu kwa msimu wa 2020-21.

"Ubora wa klabu ni matokeo chanya na si vinginevyo nina imani ndicho ambacho viongozi wetu wamekilenga kwa sasa," amesema Niyonzima

Mnyarwanda huyo ni miongoni mwa wachezaji watatu wa kigeni waliobaki kwenye kikosi cha Yanga baada ya panga kali kupitishwa

Wengine ni mlinda lango Farouk Shikhalo na beki kisiki Lamine Moro

Yanga pia imekamilisha usajili wa nyota wengine watatu wakigeni ambao ni Yacouba Soghne, Tuisila Kinda na Mukoko Tonembe

Wachezaji wazawa waliotua Yanga ni Kibwana Shomari, Yassin Mustapha, Abdallah Shaibu, Bakari Nondo Mwamnyeto, Zawadi Mauya, Farid Mussa na Waziri Junior

Mpaka sasa Yanga imesajili wachezaji wapya 10

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’