Mafanikio hayana njia za mkato

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Aug 2020
Mafanikio hayana njia za mkato

Pichani juu ni Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Yanga, akiwa na Rais wa klabu ya AS Vita Mwanamama Bestine Kazadi

Injinia Hersi alikutana mezani na Bosi huyo wa AS Vita kukamilisha usajili wa wachezaji wawili tegemeo wa miamba hao wa soka kule DR Congo

Hapa tunawazungumzia kiungo mkabaji Tonombe Mukoko na Winga Tuisila Kisinda ambao tayari ni wachezaji halali wa Yanga

Hili lilikuwa jambo ambalo hata mashabiki wa Yanga wenyewe walikuwa hawaamini kama linaweza kutokea

Na ndio maana lawama zilikuwa nyngi kwenye mitandao ya kijamii kabla ya usajili wa nyota hao kukamilishwa

Hii ndio njia sahihi ya mafanikio ambayo Yanga na GSM wameichagua kupita

Safari ilianza pale walipoingia makubaliano na La Liga kusimamia mchakato wa Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa mabingwa hao wa kihistoria

Ni njia yenye gharama kubwa lakini ndio njia sahihi, mafanikio ya kweli hayaji kwa ujanja ujanja

Ili tuweze kufika tunapopataka tunahitaji uongozi bora, benchi bora la ufundi na wachezaji wa kiwango cha juu

Kwa mwenendo huu naiona Yanga inayoingia taratibu kwenye kundi la vilabu kama TP Mazembe, Al Ahly, Zamalek, Mamelodi Sundowns, Wydad, Esperance, yaani vilabu vigogo barani Afrika ambao kila mwaka malengo yao ni kuwa mabingwa wa Afrika

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
14h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
17h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
18h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
19h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’