Kazi ndio kwanza imeanza..

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Aug 2020
Kazi ndio kwanza imeanza..

Wakati wakiweka wazi mkakati wa usajili, GSM walisema watakwenda kusajili wachezaji wa ndani daraja A na wachezaji wa nje wa daraja la juu na wakikosa angalau wa daraja B

Na wakasisitiza watatumia pesa kuwapata wachezaji hao, hilo limetimia kwa usajili wa nyota wawili kutoka AS Vita Tusila Kisinda na kiungo Mukoko Tonombe

Yanga ilihitaji winga mwenye kasi, kwa waliomfuatili Kisinda wanafahamu balaa lake

Akiwa na umri wa miaka 20 tu, Kisinda alijihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha AS Vita

Dogo ana kasi ya kimbunga, sijui wale waliosajili wachezaji wanaosubiri pensheni watammudu vipi kinda huyu

Lakini pia, Kisinda atacheza upande mmoja wa winga na ule upande mwingine atakuwepo Farid Mussa!

Mukoko ni kiungo mkabaji, huyu ni sawa na Tshishimbi wawili, tena Tshishimbi yule wa mwaka 2017 sio huyu aliyeachwa

Bado Injinia Hersi hajamaliza kufanya yake, kwani inaelezwa akitoka DR Congo anaelekea Afrika Kusini kumfuata kiungo mwingine fundi

Lakini ukiachana na Yacouba Sogne anayesubiri kutua, upo mpango wa kumsajili mshambuliaji mwingine wa daraja la juu

Hakuna shaka, furaha inarejea Jangwani...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’