Kesho Jumatatu, August 17 Bodi ya Ligi Kuu itakuwa na Mkutano na Wanahabari, mkutano ambao utatumika kuweka hadharani Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2020/21
Kulingana na taarifa iliyotolewa na TPLB, Mkutano huo utafanyika saa tano asubuhi kwenye ukumbi wa Mikutano wa TFF
"Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) itafanya mkutano na Wanahabari kesho Jumatatu saa 5:00 asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Ilala jijini Dar es Salaam"
"Lengo la mkutano huo ni kutangaza ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2020/2021," imesema taarifa ya TPLB
Mambo yameiva, hakuna mda zaidi wa kusubiri...!
ADVERTISE HERE